Thursday, 28 April 2022

Cold Chain Management


In immunization,  ensuring the potency of the vaccine is very important,  Agrey E Hyera, Health Officer and Tarime Town Immunization & Vaccine Officer repairing one of the Cold Chain Equipment in April, 2022 at Gamasara Dispensary to ensure safe storage of  vaccine at conducive environment (2°c to 8°c).
The damaged cooling unit was replaced with new one and refrigerator functioned well after repairing.


 

Sunday, 8 January 2017

UTHAMANI WA MAISHA YA MWANADAMU



Kwanza kabisa nipende kumshukuru mungu kwa kutupa kibali cha kuingia mwaka 2017. Ni wengi walipenda kuendelea kuishi, lakini hakakupata neema ya kuuona mwaka huu 2017.
katika somo letu la leo, tunakwenda kujifunza kwa habari ya uthamani wa maisha ya mwanadamu, yaani ni nini kitaifanya jamii ikuthamini.
Kumbuka, ili uthaminike mahala popote pale, ni lazima wewe mwenyewe uanze kujitamini, na yafuatayo ni mambo muhimu sana ambayo humfanya mtu awe wa thamani katika jamii yake;

1. Kumcha Mungu.


Mungu ali[pomwumba mwanadamu, alikuwa na mahusiano naye ya moja kwa moja, kama rafiki wa karibu, ndio maana hata walikuwa na wasaa wa kumtembelea.Mwanzo 3:8
pasipo kumcha Mungu, hakuna jamii itakuamini na kukuheshimu, hata jamii ya waovu inawaheshimu sana watu wanaomcha Mungu. Mithali 14:27
 
2. Akili/Hekima.


ili jamii ikuheshimu, lazima uwe na akili kichwani. Akili huleta hekima inayotuwezesha kuamua mambo. tunapokwenda shule, hiyo ni moja ya kujua mambo ili yatuongezee hekima ya kutenda, na pasipo nguvu ya Mungu, ni vigumu kuwa na hekima inayoheshimika katika jamii. Mithali 15:21
 
3. Utajiri.



imekuwa na kelele nyingi sana kupinga utajiri, hasa inapofundishwa kwa wana wa Mungu. Ila uhalisia, watu wengi ambao hupinga suala la utajiri ni wale ambao wamegubikwa na umasikini, na ibilisi amewafunga akili zao. Ili uheshimike katika jamii ni lazima uwe na uwezo kifedha, vinginevyo utaishia kudharaulika. Mithali 14:20
 
HITIMISHO.
Ili uheshimike katika jamii, lazima uwe msaada katika hiyo jamii, huwezi kuisaidia jamii endapo wewe mwenyewe unataka jamii ikusaidie, na kama unataka jamii ikusaidie jua fika huwezxi kuheshimika katika jamii hiyo.
Amua sasa kuheshimika katika jamii yako,

KHERI YA MWAKA MPYA 2017

Tuesday, 15 November 2016

KUKATA TAMAA NI DHAMBI.


Bwana Yesu asifiwe sana, mpendwa katika Bwana Yesu, naomba leo nikupe siri hii, unajua kukata tamaa ni dhambi na chukizo mbele za MUNGU??
Hebu tafakari, shetani hajawahi kukata tamaa. Wewe unapata wapi nguvu ya kukata tamaa?? Yaani leo unakemea na kufukuza pepo na kufukuza wachawi lakini kesho utakuta wako sehemu nyingine wanafanya uharibifu ule ule! Hawakati tamaa ili watimize kusudi Lao!
Ayubu pamoja na changamoto zote lakini hakuwahi kukata tamaa. Wewe ni nani mpaka ukate tamaa?? Kukata tamaa ni kumsaidia kazi shetani, yaani anakupa moyo wa kukata tamaa lakini yeye hakati tamaa!
Itamkie hiyo changamoto kwenye elimu, ndoa, Utumishi, afya, na popote kwamba MUNGU wako aliye mvusha Shadrack, Meshack na Abednego, MUNGU aliye wavusha wana wa Israel, MUNGU aliye mvusha Ayubu atakuvusha na wewe kwa jina la Yesu, amen.
Acha changamoto zikusaidie kukua kiimani na pia zikusaidie kuandaa ushuhuda wa utukufu, amen.

Wednesday, 26 October 2016

"USIJIMALIZE MWENYEWE"


Na Mtumishi Charles Francis,

Bwana YESU asifiwe sana wapendwa...
MUNGU wetu anatupenda na Roho Mtakatifu anataka tujifunze leo kwa habari ya ulimi. Kuna ufunuo wa ajabu sana ambao ukiupata utakusaidia sana. Naomba tupite kwenye maandiko yafuatayo:
ISAYA 54:17
"Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwana, kila ULIMI utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa Bwana, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema Bwana."
Iko hivi, ulimi ni silaha ya kuua na kuponya. MUNGU wetu kwa kufahamu hilo akatuonyesha kwenye Mithali 18:21, inasema "Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake".
Ukirudi kwenye andiko la Isaya 54 :17, anasema ulimi utakaoinuka juu yako utahukumiwa yaani wewe mwenyewe utatoa hukumu juu ya ulimi huo. Nataka twende taratibu kwenye ufunuo huu ili uelewe na upone.
Jiulize ni mara ngapi ulimi wako umenena madhaifu na kujitamkia maneno yasiyo faa ukadhani ni hali ya kawaida?? Sasa katika ulimwengu wa roho, hayo maneno ni silaha maana ulimi wako umetumika vibaya kinyume chako.
Ukitaka kujua kwamba ulimi ni silaha, waulize wachawi, waganga na washirikina. Utauliza mtumishi Charles namaanisha nini, sikiliza kuna kitu wanaita "kunuiza" yaani kutamka maneno magumu au mabaya juu ya mtu fulani ili asifanikiwe. Hawatamki mara moja, ni zaidi ya mara moja. Kwa kifupi kutamka jambo kwa kuweka nia ni kanuni ya ulimwengu wa roho ili nia hiyo iwe kweli na halisi katika ulimwengu wa kawaida. Wewe umejitamkia nini na mara ngapi??
Unapo ona mambo ni magumu, unapiga magoti na kuanza kutumia maandiko kumpiga adui (unajipiga mwenyewe). Hapo una hukumu ulimi wako kuwa "umekosea" na kwa maana nyingine unajishambulia bila kujua. Unaweza kuhama makanisa yote, lakini kwa jina la YESU siri hii imefunuliwa ili upone.
Na kwa kuwa MUNGU hapingani na neno lake, hivyo dunia husema "tumesikia" na MBINGU husema "amina" alafu MBINGU hukaa kimya ili dunia ifanye kazi maana MUNGU wetu ana heshimu "protocol ya uumbaji wake". Hapo ndiyo utaona sadaka unatoa, ibada unafanya, kanisani unajitoa na mchungaji anakuwekea mikono kichwani kila siku mpaka unapata "kipara" lakini mambo hayaendi. 

Na

Monday, 24 October 2016

HAKUNA KUACHA


Wagalatia 6:9 “Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho”


Wafilipi 3:13-17 “Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele; 14 nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.15 Basi sisi tulio wakamilifu na tuwaze hayo; na hata mkiwaza mengine katika jambo lo lote, Mungu atawafunulia hilo nalo. 16 Lakini, hapo tulipofika na tuenende katika lilo hilo.”

Uvumilivu na ustahimilivu ni mambo mawili yasiyoweza kutengana kamwe katika maisha ya mtu anaye mwamini Bwana Yesu. Safari ya wokovu tulioitiwa inawezekana tu kwa uvumilivu kwa sababu ni kama kukimbia mbio za riadha. Na haiwezekani kutimiza safari ya wokovu pasipo kujazwa na moyo wa ustahimilivu (Waebrania 6:12).
Ni kama ilivyo ushirika kati ya imani na ukiristo wako. Huwezi sema wewe ni mkristo na ukawa huna imani. Sishangai kuona uvumilivu umetajwa kama tunda la Roho katika Wagalatia 5:22.

Je unatambua kuwa unapojaribiwa Mungu hutumiwa hilo jaribu kutengeneza uvumilivu ndani yako? Lakini ukishindwa kulishinda hilo jaribu na ule uvumilivu hauumbiki ndani yako. Kwa sababu hii wengi waliopitia majaribu na wakashindwa kuyamudu wana nung’unika kuwa Mungu hawapendi. Na Baadhi yao huamua hata kuacha imani zao, kitendo hiki kinaenda kinyume kabisa na Neno la Mungu katika
Waebrania 6:12 “ili msiwe wavivu, bali mkawe wafuasi wa hao wazirithio ahadi kwa imani na uvumilivu”
• Wana wa Mungu lazima tujifunze kuvumilia maana Bwana amesema tutavuna tuzipozimia mioyo.
• Lazima tutambue majira na nyakati ya baraka zake kwetu. Maana Yeye anajua hata ukipewa leo utaishia wapi na hiyo mali.
• Tambua kuwa maamuzi ya Mungu hayaangalii vile unataka maana yeye anaangalia nini kitatokea kesho.
• Tambua kuwa Mungu hatakupa kamwe baraka ambayo hujajiandaa kuipokea Vinginevyo itakuua.

Ukiona jambo au baraka unayoitegemea haitimii kwako kwa muda unaotaka endelea kustahimili na kuvumilia. Hata kama ukaona jambe linapoteza matumaini wewe chukua Biblia soma na kutafakari Neno lake na Muombe Mungu akupe Neno kwa hilo...............
Na Pastor Boniface Evarist
Efatha Ministry - Mbinga

Friday, 30 September 2016

BARAKA YA YUDA





Baraka ya Yuda iko ndani ya Jina Lake. Neno Yuda Linalotokana na neno la Kiebrania yadah. Yadah maana yake ni “kustahi au kunyoosha mikono” “kukiri”, “kusifu” au “kutoa shukrani”. Jina la Yuda linamaanisha sifa. Kwa nini hii ni baraka? Kwa sababu sifa ndicho kivutio pekee kinachopelekea uwepo wa Mungu kwetu.

Mwanzo 29:35 "Akapata mimba tena, akazaa mwana. Akasema, Mara hii nitamsifu Bwana; kwa hiyo akamwita jina lake Yuda; akaacha kuzaa."

Sifa ni dawa ya Mungu ibadidirishayo Mazingira yako.
Lea angeweza kuchagua Mazingira yake, na angechagua jina ambalo hata lisingeleta baraka kwake. Elewa kabisa alikuwa hapendwi na Yakobo, alimpenda mdogo wake Raheli kuliko Lea.
Maisha ya Lea yalikuwa ya mateso sana, Mungu akaonesha rehema zake na akamruhusu Lea kuzaa watoto wakati Raheli alikuwa hazai.
Mwanzo 29:31 "Bwana akaona ya kwamba Lea hakupendwa, naye akafungua tumbo lake; bali Raheli alikuwa hazai."

Hata hili halikusababisha Yakobo kumpenda Lea. Baada ya kumpa mwanae wa kwanza jina la Reubeni-Kwa kuwa Bwana ameona teso langu (Mwanzo 29:32) –na mwana wa pili akamwita Simeoni (Mwanzo 29:33)-kwa kuwa Bwana amesikia mimi sikupendwa. Lakini Lea alipopata mtoto wa tatu Akampa jina la Yuda 
“Mwanzo 29:35 Akapata mimba tena, akazaa mwana. Akasema, Mara hii nitamsifu Bwana; kwa hiyo akamwita jina lake Yuda; akaacha kuzaa”

Bwana alifurahishwa na jina ambalo Lea alichagua kwa mtoto wake Yuda (Tazama Zaburi 78:67-68). Mungu alichagua Yuda kupokea baraka na kuwa babu wa Mfalme Daudi na Masihi

1 Mambo ya Nyakati 28:4 "Walakini Bwana, Mungu wa Israeli, alinichagua katika nyumba yote ya babangu kuwa mfalme juu ya Israeli milele, kwa kuwa amemchagua Yuda awe mkuu; na katika nyumba ya Yuda, alichagua nyumba ya babangu, na miongoni mwa wana wa babangu, aliniridhia mimi ili kunitawaza niwe mfalme juu ya Israeli wote;"

Umuhimu wa kabila la Yuda umeonekana katika Agano la kale maana walikuwa viongozi na hii baraka alitoa Yusufu alipobariki wanawe (Mwanzo 49:8-12)
Na uongozi wa kabila la Yuda pia unaonekana katika kitabu cha Waamuzi wakati makabila ya Isaraeli yanaenda vitani dhidi ya kabila la Benjamini, Mungu anaagiza kabila la Yuda liongoze vita (Waamuzi 20:18)
Baada ya kutoka utumwani katika kuweka wakfu ukuta wa Yerusalemu Bwana akaweka kwaya mbili za kabila la Yuda (Nehemia 12:27-31)
Katika Zaburi 108:8 Yuda ameelezewa kama Fimbo ya Mungu. Hapo inamaanisha Yuda ni mwakilishi wa mamlaka na nguvu ya Mungu. Na hili lilitimizwa na mfalme Daudi na waliofuatia kwake na zaidi sana Yesu Kristo.
Katika agano Jipya mamlaka ya Mungu alifunuliwa na uzao wa kabila la Yuda -
Ufunuo wa Yohana 5:5 "Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake saba."

Na hata Ufunuo 7:5 tunaona watatiwa Muhuri kwanza kabila la Yuda nyakati za Mwisho.
Kibali cha Mungu katika uzao wa Yuda tunaona pia 

Zaburi 114:2 “Yuda ilikuwa patakatifu pake, Israeli milki yake.” 

Kwa maana nyingine Mungu alionesha mamlaka yake na nguvu zake kwa Waisreali wote ila makao makuu yake na makazi yake ya kuishi yalikuwa Yuda.
Yuda iliona uwepo wa Mungu wa pekee sana kuliko kabila lolote. Yerusalem na mlima Sayuni, mlima ambapo hekalu lilisimamishwa ilikuwa ndani ya mipaka ya Yuda

Zaburi 76:1-2 “Katika Yuda Mungu amejulikana, Katika Israeli jina lake ni kuu. Kibanda chake pia kiko Salemu, Na maskani yake iko Sayuni.”

Yuda ililindwa na Mungu sana kwa sabubu ndipo palipokuwa mahali pa uwepo wake.

Na; Pastor Boniface Evarist
Efatha Ministry - Mbinga. 

Monday, 19 September 2016

KULITUMIKIA KUSUDI LA KUUMBWA KWAKO - 2


Katika toleo la mwanzo la tarehe 12 June 2016, tulianza kuona vipengele viwili vya mwanzo ambavyo ni; Kutenganisha Kati ya Mambo Yaliyo ya Haki na Maovu, pia tuliona kipengele kingine cha Kutenganisha Kati ya Mambo yaliyo Makubwa na Madogo, ya Muhimu na ya kawaida. Leo wacha tuone kipengele kingine;

3. BAINISHA MAZINGIRA ULIYO NAYO

ni lazima utambue mazingira ya aina gani yamekuzunguka, na jambo gani unaweza kulitenda katika mazingira hayo.
lengo la kubainisha mazingira si ili kukukatisha tamaa, au kuona ni namna gani umezungukwa na mazingitra magumu, tambua hakuna gumu la kumshinda bwana yesu, Yeye akiwa ndani yako basi nawe hakuna la kukushinda. lengo la kubainisha mazingira haya ni ili ujue namna ya kupanga mikakati yako na kuitengeleza kwa matokeo chanya.
Bainisha pia majira ya kila jambo katika mikakati yako, ni muda gani ufanye jambo gani, kwa ujumla zitambue rasilimali zinazokuzunguka ikiwa na pamoja na namna ya kuzitumia rasilimali hizo.
tunasoma;
Mwanzo 1:9-13 "Mungu akasema, “Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, nchi kavu itokee.” Ikawa hivyo. Mungu akapaita mahali pakavu “Nchi” na kusanyiko la maji akaliita “Bahari.” Mungu akaona kuwa ni vyema. Kisha Mungu akasema, “Nchi na ioteshe mimea. Mimea izaayo mbegu, na miti izaayo matunda yenye mbegu.” Ikawa hivyo. Basi, nchi ikaotesha mimea izaayo mbegu kwa jinsi yake, na miti izaayo matunda yenye mbegu kwa jinsi yake. Mungu akaona kuwa ni vyema. Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya tatu."

Saturday, 17 September 2016

KUFIKIA DARAJA LA JUU



Mambo ya umuhimu kujifunza ili kufikia Daraja la juu.

I. Mtambue kamanda mkuu mbele yako


II. Jua kuishika amri yake


III. Jua kutekeleza kila amri kwa haraka na kwa ubora


IV. Jifunze kumshukuru Mungu 


Kwa maana ni kwa Neema tu...mbele ya bosi wako,kiongozi wako n.k


Utaaminiwa na yeye aliye juu na kukupatia Kigali cha kuingia na kutoka kwa furaha kuliko wengine.Ili litimie neno linalosema 'amenipaka mafuta ya furaha kuliko wengine'

Pastor Phillipo Guni,
Efatha Ministry - Ruvuma

Monday, 29 August 2016

SIRI KUBWA YA MAFANIKIO

SIRI KUBWA YA MAFANIKIO
Wapendwa wangu wakubwa wa blog hii, asante kwa kuendelea kuwa nami kwa kufuatilia masomo na jumbe mbalimbali zinazotolewa katika blog hii.
Leo nimeona ni vizuri nikawashirikisha siri hii kubwa ya mafanikio kwani imekuwa ikiwasumbua wengi na hata kuwaharibia wengine mstakabali wa maisha yao.
Nimefikia hatua hii ya kuweza kuandika ujumbe huu, kwani kwa ujumla katika maisha yangu, kuna mambo mengi sana ambayo nimekuwa nikidhamiria kwa moyo wangu yakifanikiwa, yawe makubwa au madogo.
Siri hiyo kubwa ni ipi?
1.       Mwamini Mungu na mtegemee Yeye.
Neno la Mungu limetuasa sana juu ya kuwategemea wanadamu.
 Yeremia 17:5 “Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana”
Kamwe usitegemee kuwa mwanadamu atakufikisha kunako mafanikio yako. Kumbuka mwanadamu anaweza kubadilika muda wowote, Mungu peke yake si kigeu geu. Ukitaka kuamini kuwa mwanadamu hawezi kukufikisha katika mafanikio yako, ngoja ufanikiwe uwe sawa nay eye au umzidi ndipo utakapotambua.
Kumbuka: Mungu huweza kumtumia mwanadamu katika kukufanikishia, usiitoe imani yako kwa Mungu.
2.       Jiwekee malengo
Ili kuleta mafanikio, lazima uwe na dira inayokuongoza kuwa ni wapi unataka kuelekea. Jiwekee malengo na hakikisha unasimamia malengo yako kwa gharama yoyote ile. Utakutana na mengi katika kuyatekeleza malengo hayo, wengine wakikutia moyo na wengine wakikukatisha tamaa ila usikate tama wala kupoteza mwelekeo katika malengo yako.
Yeremia 31:21 “Jiwekee alama za njia; jifanyie miti ya kukuongoza; uuelekeze moyo wako kwenye njia kuu, njia ile ile uliyoiendea; rudi tena, Ee bikira wa Israeli, irudie hii miji yako.”
Naikumbuka kauli ya mwalimu wangu wa shule ya Msingi, Mwl Athumani Z. Ngonyani; “Kupanga ni kulazimisha mafanikio.” Itumie kauli hii, itakusaidia. Wakati wengine wanasema huwezi, wewe ng’ang’ana kuyatimiza malengo yako, waje kuona mafanikio.
3.       Jiamini, amini kuwa unaweza.
Usisubiri watu wa kukutia moyo ndipo uamini kuwa unaweza, amini kuwa hadi ukawa na wazo hilo au ukawiwa kulitenda jambo hilo, ni uthibitisho tosha kuwa jambo hilo unaliweza ni saizi yako.
Hakuna mwanadamu anayetambua uwezo ulio nao, au ni jambo lipi unalihitaji, ni Mungu peke yake na wewe mwenyewe ndio mnaofahamu, acha kupoteza muda kwa kuyafuatilia maneno ya watu, yatakuchelewesha kunako mafanikio yako. Maneno yao yawe sababu ya kukuongezea juhudi katika kutekeleza mpango uliojiwekea,

Sunday, 12 June 2016

KULITUMIKIA KUSUDI LA KUUMBWA KWAKO


Kutofanikiwa nkatika jambo lolote ni dalili tosha ya kutokuwa na Mungu, yaani kuyatenda mambo pasipo maongozi ya Roho Mtakatifu.
Hesabu 23:19 "Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza?"

Ili kufanikiwa kulitumikia kusudi la kuumbwa kwako, inategemea sana na maamuzi yako na namna unavyoenenda. Watu wengi wamejikuta wakitembea duniani hadi mauti ikiwafikia pasipo kujua ni nini hasa walipaswa kutenda.
Katika makala zilizopita tuliona namna mtu anaweza kulitambua kusudi la kuumbwa kwake, leo tunaendelea na namna ya kulitimiza kusudi hilo baada ya kulitambua;

1. KUTENGANISHA KATI YA MAMBO YALIYO YA HAKI NA MAOVU.

Katika toleo lililopita tuliona umuhimu wa maarifa katika kusudi unalopaswa kulitimiza, katika hatua hiyo ya kuwa na maarifa, pia ni muhimu sana kutambua mambo yaliyo ya haki na yasiyo ya haki. Ni vyema kujitenga na uovu tangu mwanzo, kwani mwanzo ndio msingi ambao unaonesha mwelekeo wa kule unaelekea.
Kutojitenga na uovu itakupelekea kutokuwa na mwisho mzuri, kwani huwezi pata jengo zuri la nyumba toka katika msingi mbovu. Hii ni pamoja na marafiki wasiofaa, na kila jamii ambayo itakupelekea kuanko uharibifu. Ndio maana hata katika uumbaji, baada ya Bwana Mungu  kuziumba Mbingu na Nchi, hatua iliyofuata ni kutenganisha kati ya nuru na giza, tunasoma;

Mwanzo 1:1-5 "Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza. Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja." 

2. KUTENGANISHA MAMBO MAKUBWA NA MADOGO/MUHIMU NA YA KAWAIDA.

Ili kufanikiwa, ni lazima uwe na mpango kazi, katika mpango kazi lazima upange mambo yako kwa vipaumbele, onesha mambo makubwa na madogo, yaliyo muhimu na yale ya kawaida. Hii itakusaidia kutambua ni mambo gani uanze nayo na yapi ni ya muhimu, yaani lazima yatekelezwe. Kutoainisha mambo muhimu ya kuyatekeleza imepelekea watu wengi kupoteza muda mwingi katika kutenda mambo ambayo hata hayana umuhimu, yaanio si ya lazima na kuacha kufanya yaliyo ya lazima. Katika Biblia tunasoma pia baada ya kutenga giza na nuru, Bwana Mungu aliumba anga na kutenganisha kati ya maji ya angani na yale ya nchini ya anga.

Mwanzo 1:6-8 " Mungu akasema, Na liwe anga katikati ya maji, likayatenge maji na maji. Mungu akalifanya anga, akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; ikawa hivyo. Mungu akaliita lile anga Mbingu. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya pili." 

Ni lazima ujue kutofautisha kati ya mambo ya juu (makubwa/muhimu) na yale ya chini (madogo/ya kawaida)

~tuonane katika toleo lijalo~

Wednesday, 27 April 2016

MAMBO MUHIMU KATIKA KUFIKIA MAFANIKIO ~ TOLEO MAALUMU



Ni miaka nane sasa tangu niokoke na kujiunga na kanisa la Efatha tarehe 27 Aprili 2008. Sijawahi kujutia maamuzi haya, zaidi sana naona kuwa bado sijafikia viwango nilivyokusudiwa. Nakaza mwendo nifikie viwango nilivyokusudiwa ili nipate kutimiza kusudi la kuumbwa kwangu. Leo napenda kuwashirikisha mambo yafuatayo ambayo ni muhimu kuyatambua katika kufikia mafanikio yako;

1.      KUWATAMBUA WATU SAHIHI KWAKO;
Kuna watu ambao unaweza kutana nao katika maisha yako, ukawaona kuwa ni watu muhimu sana na kiukweli wakafanyika msaada kwa namna moja au nyingine katika maisha yako, lakini watu hao hao wakafanyika uharibifu mkubwa sana.
Kumbuka kuwa shetani anapotaka kukuangamiza hatokuja na mambo mabaya tu, atakuletea mambo mazuri lakini ndani yake anachanganya na uharibifu kwa ajili ya kukuangamiza. Kuwa makini sana na watu wa aina hii, watu hawa ndio wale wanaotamkwa kuvaa ngozi ya kondoo wakati ndani yao ni mbwa mwitu. Mwombe Mungu akukutanishe na watu sahihi kwako.

2.      KUWEKA MATUMAINI MAHALA SAHIHI;
Matumaini yako; hiki pia ni kipengele muhimu sana, lazima ujue ni nani unamtumainia katika maisha yako. Kuwatumainia wanadamu hata kama wanamsaada mkubwa sana katika maisha yako ni kutafuta mauti yako, kumbuka umeumbwa na Mungu kwa kusudi lake, hivyo basi Mungu hahitaji kutafutiwa watu wa kumsaidia kutimiza kusudi lake, yeye anao wengi. Hata katika maisha yako, si wewe unayemtumia Mungu kutimiza kusudi lako, bali ni Mungu anakutumia wewe kutimiza kusudi lake. Biblia pia inasema amelaaniwa mtu Yule amtegemeaye mwanadamu na amebarikiwa mtu Yule amtegemeaye Bwana.

3.      KUJIAMINI;
 Kutojiamini na kutothubutu, kipengele hiki ni kibaya sana, kwani hata kama una uwezo mkubwa kiasi gani, endapo utakosa kujiamini nma kuthubutu hakuna kitu kitatokea katika maisha yako. Kutojiamini ni sawa na kuwa na risasi pasipo bunduki, na kutothubutu ni sawa na kuwa na risasi na bunduki lakini kutofyatua risasi ili kusababisha jambo litokee.

4.      KUWA NA MAARIFA;
 Watu wengi sana wamekuwa wavivu wa kutafuta maarifa, hupenda sana wengine wawatafutie taarifa na kuwasimulia. Kamwe hutoendelea kwa kutegemea wengine wakutafutie taarifa na kukusimulia. Huwezi kukua kiroho kwa kusubiri Mchungaji wako au kiongozi wako yeyote wa kiroho akusomee Biblia siku za Ibada na kukutafsiria, ni lazima uchukue hatua wewe mwenyewe ya kumtafuta Mungu kwa juhudi. Wengine pia wanaona njia rahisi ni kukimbilia kusoma vitabu vilivyoandikwa na watumishi mbali mbali hasa vikiwa na kurasa chache kwa sababu ya uvivu wa kusoma Biblia yenye vitabu vingi. Huwezi kukua kwa staili hii, kwani si kila kitabu kilichoandikwa na mtumishi wa Mungu kipo sahihi, ni kwa wewe mwenyewe kuchukua hatua ya kusoma Biblia na kumwomba Roho Mtakatifu akusaidie ndio itakupa ufahamu wa juu. Hata utakaposoma vitabu mbalimbali vya watumishi, utaweza kutambua sehemu ambazo hazijaandikwa kwa usahihi.
Katika jambo lolote, tafuta maarifa wewe mwenyewe, usisubiri kusimuliwa na wengine, chukua hatua.

5.      KUPENDA URAHISI/UVIVU;
Kupenda njia rahisi, watu wengi hupenda kupata mambo kirahisi rahisi, kumbuka kuwa umeumbwa kwa kusudi la Mungu, usiwe kigeugeu katika kulitimiza kusudi hilo, unaona ndani yako una wito wa kumtumikia Mungu, lakini ukiangalia mazingira unayaona magumu kwa macho yako ya klibinadamu na unatakata kuacha ili uende kwenye jambo jingine, jiulize hilo unalotaka kulikimbilia ni kusudi la nani? Mungu amekuita kwenye kusudi lipi? Usiutoroke wito ulioitiwa, kwani katika wito ulioitiwa utapaswa kutoa hesabu siku ya mwisho.

"Binafsi napenda kuwashukuru sana wale wote waliofanyika msaada kwangu kwa namna moja au nyingine,bado natambua sana mchango wenu kwangu, Wazazi wangu, Mwl. Athuman Z Ngonyani, Mr. & Mrs Kattanga, Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira na watumishi wote ndani ya Huduma ya Efatha, Uncle Gaston A. Nchimbi,Mr. Amon Mandele, Mr. John Sweke, Mr. Kachingwe Kaselenge, Ndugu zangu, jamaa na marafiki, natambua mchango wenu,  Mungu asiwapungukie kwa wingi wa baraka zake; Amina."

Saturday, 16 April 2016

NGUVU YA MAARIFA - SEHEMU YA PILI


 Maarifa yana nafasi kubwa sana kubadili maisha yako, msingi wa maisha yako na mafanikio yake iwe Kiroho, Kiuchumi, Kifamilia, Ndoa, Kazi yako au jambo lolote lile hutegemea sana maarifa uliyonayo katika jambo hilo, epuka kuhifadhi taarifa zisizo sahihi kwani zitafanyika uharibifu kwako. Kwa gharama yoyote ile hakikisha unahifadhi taarifa chanya na achana na taarifa hasi, epuka ushauri wa walioshindwa na kukata tamaa, na jifunze kwa waliofanikiwa katika changamoto na kutimiza malengo na maono waliyonayo.


MAHUSIANO YALIYOPO KATI YA IMANI NA MAARIFA.

Kama tulivyojifunza toka katika toleo lililopita kuwa; Maarifa ni uhalisia, taarifa na ujuzi anaoupata mtu kupitia uzoefu au elimu; ni dhahania au kwa kulitenda jambo. Pia maana ya Imani kama ilivyoelezwa ki-Biblia;

Waebrania 11:1 "Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana"


Imani ni sehemu ya maarifa aliyonayo mtu, kwani katika maarifa tunaona neno DHAHANIA, ambapo katika Waebrania linaelezwa kama mambo yanayotarajiwa na mambo yasiyoonekana.
Imani ya mtu inategemea sana maarifa aliyonayo, kwani Imani hutokana na kile ambacho ufahamu wa mtu umekipokea yaani maarifa aliyonayo. tunasoma;

Warumi 10:17 "Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo."

Hii inaonyesha kuwa ili mtu aweze kuamini, lazima apate maarifa ya kumuwezesha kuamini. Huwezi kuamini kitu ambacho hakipo akilini mwako, ndio maana mtu ili aamini, anahitaji aisikie Injili ya Neno la Kristo ili apate kuamini, tunasoma;

Marko 16:15-16 "Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa."

Tumeona Ki-Biblia Mahusiano yaliyopo kati ya Maarifa na Imani, Kweli isiyofahamika kwa mtu; mtu huyo hawezi kuiamini, kwani ni kitu ambacho hakipo kabisa katika ufahamu wake. Pia kupata maarifa na kuamini ni vitu viwili tofauti, kwani wengine hupata maarifa lakini mioyo yao haipo tayari kuamini. Unaweza kukutana na mtu anayafahamu maandiko ya kwenye Biblia vizuri sana, ila hakuna anachoamini toka katika maandiko hayo ya kwenye Biblia.

Mathayo 13:14-15 "Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likisema, Kusikia mtasikia, wala hamtaelewa; Kutazama mtatazama, wala hamtaona. Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya."

Tunaona dhahiri katika mtiririko huu kuwa kuna hatua ya kusikia na kuona ambayo ni sawa na kupokea maarifa, lakini hatua ya kuongoka ambayo ni matokeo ya kuamini kilichosikiwa au kilichoonwa.
Imani ni kweli, thabiti, hivyo imani yako ili isiwe potofu ni lazima iwe KWELI. Kwani kama mtu ameamua kuamini kitu au jambo ambalo si kweli, imani hiyo huitwa imani potofu.

~ BARIKIWA SANA!! ~
 Kwa maoni au ushauri wasiliana nami; agreyndiwu@gmail.com Simu; +255 71 346 9596