Wagalatia 6:9 “Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho”
Wafilipi 3:13-17 “Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele; 14 nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.15 Basi sisi tulio wakamilifu na tuwaze hayo; na hata mkiwaza mengine katika jambo lo lote, Mungu atawafunulia hilo nalo. 16 Lakini, hapo tulipofika na tuenende katika lilo hilo.”
Uvumilivu na ustahimilivu ni mambo mawili yasiyoweza kutengana kamwe
katika maisha ya mtu anaye mwamini Bwana Yesu. Safari ya wokovu
tulioitiwa inawezekana tu kwa uvumilivu kwa sababu ni kama kukimbia mbio
za riadha. Na haiwezekani kutimiza safari ya wokovu pasipo kujazwa na
moyo wa ustahimilivu (Waebrania 6:12).
Ni kama ilivyo ushirika kati ya imani na ukiristo wako. Huwezi sema wewe ni mkristo na ukawa huna imani. Sishangai kuona uvumilivu umetajwa kama tunda la Roho katika Wagalatia 5:22.
Je unatambua kuwa unapojaribiwa Mungu hutumiwa hilo jaribu kutengeneza uvumilivu ndani yako? Lakini ukishindwa kulishinda hilo jaribu na ule uvumilivu hauumbiki ndani yako. Kwa sababu hii wengi waliopitia majaribu na wakashindwa kuyamudu wana nung’unika kuwa Mungu hawapendi. Na Baadhi yao huamua hata kuacha imani zao, kitendo hiki kinaenda kinyume kabisa na Neno la Mungu katika
Waebrania 6:12 “ili msiwe wavivu, bali mkawe wafuasi wa hao wazirithio ahadi kwa imani na uvumilivu”
• Wana wa Mungu lazima tujifunze kuvumilia maana Bwana amesema tutavuna tuzipozimia mioyo.
• Lazima tutambue majira na nyakati ya baraka zake kwetu. Maana Yeye anajua hata ukipewa leo utaishia wapi na hiyo mali.
• Tambua kuwa maamuzi ya Mungu hayaangalii vile unataka maana yeye anaangalia nini kitatokea kesho.
• Tambua kuwa Mungu hatakupa kamwe baraka ambayo hujajiandaa kuipokea Vinginevyo itakuua.
Ukiona jambo au baraka unayoitegemea haitimii kwako kwa muda unaotaka endelea kustahimili na kuvumilia. Hata kama ukaona jambe linapoteza matumaini wewe chukua Biblia soma na kutafakari Neno lake na Muombe Mungu akupe Neno kwa hilo...............

Na Pastor Boniface Evarist
Efatha Ministry - Mbinga
No comments:
Post a Comment