Wednesday, 26 October 2016

"USIJIMALIZE MWENYEWE"


Na Mtumishi Charles Francis,

Bwana YESU asifiwe sana wapendwa...
MUNGU wetu anatupenda na Roho Mtakatifu anataka tujifunze leo kwa habari ya ulimi. Kuna ufunuo wa ajabu sana ambao ukiupata utakusaidia sana. Naomba tupite kwenye maandiko yafuatayo:
ISAYA 54:17
"Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwana, kila ULIMI utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa Bwana, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema Bwana."
Iko hivi, ulimi ni silaha ya kuua na kuponya. MUNGU wetu kwa kufahamu hilo akatuonyesha kwenye Mithali 18:21, inasema "Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake".
Ukirudi kwenye andiko la Isaya 54 :17, anasema ulimi utakaoinuka juu yako utahukumiwa yaani wewe mwenyewe utatoa hukumu juu ya ulimi huo. Nataka twende taratibu kwenye ufunuo huu ili uelewe na upone.
Jiulize ni mara ngapi ulimi wako umenena madhaifu na kujitamkia maneno yasiyo faa ukadhani ni hali ya kawaida?? Sasa katika ulimwengu wa roho, hayo maneno ni silaha maana ulimi wako umetumika vibaya kinyume chako.
Ukitaka kujua kwamba ulimi ni silaha, waulize wachawi, waganga na washirikina. Utauliza mtumishi Charles namaanisha nini, sikiliza kuna kitu wanaita "kunuiza" yaani kutamka maneno magumu au mabaya juu ya mtu fulani ili asifanikiwe. Hawatamki mara moja, ni zaidi ya mara moja. Kwa kifupi kutamka jambo kwa kuweka nia ni kanuni ya ulimwengu wa roho ili nia hiyo iwe kweli na halisi katika ulimwengu wa kawaida. Wewe umejitamkia nini na mara ngapi??
Unapo ona mambo ni magumu, unapiga magoti na kuanza kutumia maandiko kumpiga adui (unajipiga mwenyewe). Hapo una hukumu ulimi wako kuwa "umekosea" na kwa maana nyingine unajishambulia bila kujua. Unaweza kuhama makanisa yote, lakini kwa jina la YESU siri hii imefunuliwa ili upone.
Na kwa kuwa MUNGU hapingani na neno lake, hivyo dunia husema "tumesikia" na MBINGU husema "amina" alafu MBINGU hukaa kimya ili dunia ifanye kazi maana MUNGU wetu ana heshimu "protocol ya uumbaji wake". Hapo ndiyo utaona sadaka unatoa, ibada unafanya, kanisani unajitoa na mchungaji anakuwekea mikono kichwani kila siku mpaka unapata "kipara" lakini mambo hayaendi. 

Na

No comments:

Post a Comment