Bwana Yesu asifiwe sana, mpendwa katika Bwana Yesu, naomba leo nikupe siri hii, unajua kukata tamaa ni dhambi na chukizo mbele za MUNGU??
Hebu tafakari, shetani hajawahi kukata tamaa. Wewe unapata wapi nguvu ya kukata tamaa?? Yaani leo unakemea na kufukuza pepo na kufukuza wachawi lakini kesho utakuta wako sehemu nyingine wanafanya uharibifu ule ule! Hawakati tamaa ili watimize kusudi Lao!
Ayubu pamoja
na changamoto zote lakini hakuwahi kukata tamaa. Wewe ni nani mpaka
ukate tamaa?? Kukata tamaa ni kumsaidia kazi shetani, yaani anakupa moyo
wa kukata tamaa lakini yeye hakati tamaa!
Itamkie hiyo changamoto kwenye elimu, ndoa, Utumishi, afya, na popote kwamba MUNGU wako aliye mvusha Shadrack, Meshack na Abednego, MUNGU aliye wavusha wana wa Israel, MUNGU aliye mvusha Ayubu atakuvusha na wewe kwa jina la Yesu, amen.
Acha changamoto zikusaidie kukua kiimani na pia zikusaidie kuandaa ushuhuda wa utukufu, amen.

No comments:
Post a Comment