Katika toleo la mwanzo la tarehe 12 June 2016, tulianza kuona vipengele viwili vya mwanzo ambavyo ni; Kutenganisha Kati ya Mambo Yaliyo ya Haki na Maovu, pia tuliona kipengele kingine cha Kutenganisha Kati ya Mambo yaliyo Makubwa na Madogo, ya Muhimu na ya kawaida. Leo wacha tuone kipengele kingine;
3. BAINISHA MAZINGIRA ULIYO NAYO
ni lazima utambue mazingira ya aina gani yamekuzunguka, na jambo gani unaweza kulitenda katika mazingira hayo.
lengo la kubainisha mazingira si ili kukukatisha tamaa, au kuona ni namna gani umezungukwa na mazingitra magumu, tambua hakuna gumu la kumshinda bwana yesu, Yeye akiwa ndani yako basi nawe hakuna la kukushinda. lengo la kubainisha mazingira haya ni ili ujue namna ya kupanga mikakati yako na kuitengeleza kwa matokeo chanya.
Bainisha pia majira ya kila jambo katika mikakati yako, ni muda gani ufanye jambo gani, kwa ujumla zitambue rasilimali zinazokuzunguka ikiwa na pamoja na namna ya kuzitumia rasilimali hizo.
tunasoma;
Mwanzo 1:9-13 "Mungu akasema, “Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, nchi kavu itokee.” Ikawa hivyo. Mungu akapaita mahali pakavu “Nchi” na kusanyiko la maji akaliita “Bahari.” Mungu akaona kuwa ni vyema. Kisha Mungu akasema, “Nchi na ioteshe mimea. Mimea izaayo mbegu, na miti izaayo matunda yenye mbegu.” Ikawa hivyo. Basi, nchi ikaotesha mimea izaayo mbegu kwa jinsi yake, na miti izaayo matunda yenye mbegu kwa jinsi yake. Mungu akaona kuwa ni vyema. Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya tatu."
No comments:
Post a Comment