Baraka ya Yuda iko ndani ya Jina
Lake. Neno Yuda Linalotokana na neno la Kiebrania yadah. Yadah maana yake ni
“kustahi au kunyoosha mikono” “kukiri”, “kusifu” au “kutoa shukrani”. Jina la
Yuda linamaanisha sifa. Kwa nini hii ni baraka? Kwa sababu sifa ndicho kivutio
pekee kinachopelekea uwepo wa Mungu kwetu.
Mwanzo 29:35 "Akapata mimba tena,
akazaa mwana. Akasema, Mara hii nitamsifu Bwana; kwa hiyo akamwita jina lake
Yuda; akaacha kuzaa."
Sifa ni dawa ya Mungu ibadidirishayo Mazingira yako.
Lea angeweza kuchagua Mazingira
yake, na angechagua jina ambalo hata lisingeleta baraka kwake. Elewa kabisa
alikuwa hapendwi na Yakobo, alimpenda mdogo wake Raheli kuliko Lea.
Maisha ya Lea yalikuwa ya mateso
sana, Mungu akaonesha rehema zake na akamruhusu Lea kuzaa watoto wakati Raheli
alikuwa hazai.
Mwanzo 29:31 "Bwana akaona ya kwamba Lea hakupendwa, naye
akafungua tumbo lake; bali Raheli alikuwa hazai."
Hata hili halikusababisha Yakobo
kumpenda Lea. Baada ya kumpa mwanae wa kwanza jina la Reubeni-Kwa kuwa Bwana
ameona teso langu (Mwanzo 29:32) –na mwana wa pili akamwita Simeoni (Mwanzo
29:33)-kwa kuwa Bwana amesikia mimi sikupendwa. Lakini Lea alipopata mtoto wa
tatu Akampa jina la Yuda
“Mwanzo 29:35 Akapata mimba tena, akazaa mwana.
Akasema, Mara hii nitamsifu Bwana; kwa hiyo akamwita jina lake Yuda; akaacha
kuzaa”
Bwana alifurahishwa na jina ambalo
Lea alichagua kwa mtoto wake Yuda (Tazama Zaburi 78:67-68). Mungu alichagua
Yuda kupokea baraka na kuwa babu wa Mfalme Daudi na Masihi
1 Mambo ya Nyakati 28:4 "Walakini
Bwana, Mungu wa Israeli, alinichagua katika nyumba yote ya babangu kuwa mfalme
juu ya Israeli milele, kwa kuwa amemchagua Yuda awe mkuu; na katika nyumba ya
Yuda, alichagua nyumba ya babangu, na miongoni mwa wana wa babangu, aliniridhia
mimi ili kunitawaza niwe mfalme juu ya Israeli wote;"
Umuhimu wa kabila la Yuda umeonekana
katika Agano la kale maana walikuwa viongozi na hii baraka alitoa Yusufu
alipobariki wanawe (Mwanzo 49:8-12)
Na uongozi wa kabila la Yuda pia unaonekana katika kitabu cha Waamuzi wakati makabila ya Isaraeli yanaenda vitani dhidi ya kabila la Benjamini, Mungu anaagiza kabila la Yuda liongoze vita (Waamuzi 20:18)
Na uongozi wa kabila la Yuda pia unaonekana katika kitabu cha Waamuzi wakati makabila ya Isaraeli yanaenda vitani dhidi ya kabila la Benjamini, Mungu anaagiza kabila la Yuda liongoze vita (Waamuzi 20:18)
Baada ya kutoka utumwani katika
kuweka wakfu ukuta wa Yerusalemu Bwana akaweka kwaya mbili za kabila la Yuda
(Nehemia 12:27-31)
Katika Zaburi 108:8 Yuda ameelezewa
kama Fimbo ya Mungu. Hapo inamaanisha Yuda ni mwakilishi wa mamlaka na nguvu ya
Mungu. Na hili lilitimizwa na mfalme Daudi na waliofuatia kwake na zaidi sana
Yesu Kristo.
Katika agano Jipya mamlaka ya Mungu
alifunuliwa na uzao wa kabila la Yuda -
Ufunuo wa Yohana 5:5 "Na mmojawapo wa
wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la
Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake saba."
Na hata Ufunuo 7:5 tunaona watatiwa
Muhuri kwanza kabila la Yuda nyakati za Mwisho.
Kibali cha Mungu katika uzao wa Yuda
tunaona pia
Zaburi 114:2 “Yuda ilikuwa patakatifu pake, Israeli milki yake.”
Kwa maana nyingine Mungu alionesha mamlaka yake na nguvu zake kwa Waisreali wote
ila makao makuu yake na makazi yake ya kuishi yalikuwa Yuda.
Yuda iliona uwepo wa Mungu wa pekee
sana kuliko kabila lolote. Yerusalem na mlima Sayuni, mlima ambapo hekalu
lilisimamishwa ilikuwa ndani ya mipaka ya Yuda
Zaburi 76:1-2 “Katika Yuda Mungu amejulikana,
Katika Israeli jina lake ni kuu. Kibanda chake pia kiko Salemu, Na maskani
yake iko Sayuni.”
Yuda ililindwa na Mungu sana kwa sabubu ndipo palipokuwa mahali pa uwepo wake.
Na; Pastor Boniface Evarist
Efatha Ministry - Mbinga.