Friday, 24 April 2015

KUTAMBUA KUSUDI LA KUUMBWA KWAKO; ~inaendelea~…



Tumeona hatua ya kwanza kabisa katika kutambua kusudi la kuumbwa kwako ambayo ni Kuokoka; karibu tuendelee kufuatilia hatua nyingine za kutambua kusudi la kuumbwa kwako;


Jambo la Pili; Historia ya kuzaliwa kwako;

Historia ya kuzaliwa kwako ni ya muhimu sana, kwani kwa kiasi kikubwa huelezea mwelekeo wako. Ninaposema Historia ya kuzaliwa kwako, haijalishi kuwa historia yako ni mbaya au nzuri, bali pia hubeba kusudi la kuzaliwa kwako. Ni vizuri ukatambua historia yako, kwani ina mchamngo mkubwa sana na itakufumbua macho ni nini cha kufanya au kusudi unalopaswa kulitimiza.

Tunasoma historia ya Yakobo;

Mwanzo 25: 24-26 “Siku zake za kuzaa zilipotimia, tazama! Mapacha walikuwamo tumboni mwake. Wa kwanza akatoka, naye alikuwa mwekundu mwili wote kama vazi la nywele. Wakamwita jina lake Esau. Baadaye ndugu yake akatoka na mkono wake unamshika  Esau kisigino. Akaitwa jina lake Yakobo. Isaka alikuwa mwenye miaka sitini mkewe alipowazaa.”


Hosea 12:3 “Tumboni alimshika ndugu yake kisigino; Na alipokuwa mtu mzima alikuwa na uwezo kwa Mungu”


Hii inaonyesha ni namna gani kuzaliwa kwa Yakobo kulileta maana ya kuumbwa kwake, ndiye uzao wa taifa takatifu la Israeli, na alipewa jina hilo kutokana na uwezo aliokuwa nao.


Mwanzo 32:28 “Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda.”


Tuone pia historia ya Bwana Yesu;

Luka 2:6-7 “Ikawa, katika kukaa huko, siku zake za kuzaa zikatimia, akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng’ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.”


Tunaona kuwa Bwana Yesu mwenyewe hakupata nyumba wakati anazaliwa, kwa namna ya kibinadamu unaweza kuona kuwa alizaliwa katika mazingira magumu, lakini hii ina maana kubwa sana sawasawa na kusudi lake la kuja ulimwenguni. Ndio maana nimeandika jambo la kwanza kabisa ni kuokoka, kwani ukisharudisha mahusiano yako na Mungu, atakujulisha na kukufunulia yote kwa Roho wake Mtakatifu kwa habari ya historia ya kuzaliwa kwako. Haijalishi iwapo historia yako ni nzuri sana au ni mbaya sana, haijalishi kuwa umezaliwa katika mazingira gani, tambua kuwa historia ya kuzaliwa kwako ina kusudi la Ki-Mungu ndani yake.


Je, unaifahamu vizuri historia ya kuzaliwa kwako? Unalitambua kusudi lililobebwa katika historia hiyo?


Maombi:

“Bwana Yesu, ninakushukuru kwa kuwa Umeniumba kwa kusudi, asante kwa kunipa kufahamu kuwa namna ya kuzaliwa kwangu imebeba pia kusudi la kuumbwa kwangu; Ninakuomba Ee Bwana Yesu, kwa Roho wako Mtakatifu unifunulie yale nisiyoyajua, nipe kulitambua kusudi lililopo kwa namna ya kuzaliwa kwangu, ili nipate kutimiza mapenzi yako, nitie nguvu Bwana na nipe kuufikia mwisho mzuri; Amina.”


Kwa maswali, maoni au ushauri, tafadhali tuwasiliane;
0713469596 au agreyndiwu@gmail.com


Tukutane wakati ujao kwa kuitazama hatua nyingine itakayokuwezesha kutambua kusudi la kuumbwa kwako.


~BARIKIWA SANA~

Tuesday, 21 April 2015

NAMNA YA KUTAMBUA KUSUDI LA KUUMBWA KWAKO






Watu wengi hujiuliza sana, ni namna gani wataweza kutambua kusudi la kuumbwa kwao? Imefikia kipindi wengine wakadhani kuwa vile wanavyoishi ndio kusudi la kuumbwa kwao, hebu fuatana name ili uweze kujifunza namna utakavyoweza kutambua kusudi la kuumbwa kwako;

Kwanza kabisa, kusudi la Mungu kumuumba mwanadamu ni ili kuwa na ushirika (campany), ndio maana katika uumbaji wa Mungu, ni mwanadamu tu ndiye aliyemuumba kwa mfano na sura yake, si wanyama, si mimea, si wadudu wala si malaika.


Mwanzo 1:26 “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu;…"


 Hivyo, alimuumba mwanadamu kwa mfano na sura yake ili kupata ushirika. Ndio maana Mungu alikuwa na utaratibu wa kumtembelea mwanadamu aliyemuumba kwa mfano na kwa sura Yake.


Mwanzo 3:8 “Kisha wakasikia sauti ya BWANA Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, BWANA Mungu asiwaone.”


Hii inaonyesha kuwa Mungu alikuwa na utaratibu wa kumtembelea Adamu na mkewe katika bustani aliyowapa ili wailime na kuitunza. Wakati wa jua kupunga ni wakati wa mapumziko, hivyo BWANA Mungu alimtembelea mwanadamu aliyemuumba kwa mfano na sura yake wakati huo kwani alijua kwa wakati huo mwanadamu atakuwa katika mapumziko.


Sasa basi, kama kusudi la kwanza la uumbaji wa Mungu ni kuwa na ushirika na wewe, Je! Utawezaje kuwa na ushirika na Mungu?

Tumeona Mwanzo 3:8 hapo juu inavyoeleza, ni ukweli usiopingika kuwa dhambi huondoa ushirika wa mwanadamu na Mun gu, na ushirika huo ulivunjwa na mwanadamu mwenyewe aliyemuumba kwa mfano na sura yake, tunasoma; “… Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, BWANA Mungu asiwaone” hivyo aliyetoroka na kujificha ili kuharibu ule ushirika ni mwanadamu.

Sasa tunawezaje kurudisha ule ushirika?


Njia ya kurudisha ule ushirika ni moja tu, hakuna njia nyingine zaidi ya hiyo, ni kumpokea Yeye ( BWANA wetu Yesu Kristo wa Nazareth) aliyekubali kujitoa, kuvaa namna ya ubinadamu, kubeba dhambi ya uovu wetu ili sisi tuhesabiwe haki na kurudishiwa ushirika wetu ambao tuliupoteza.


1Timotheo 2:5 “Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Yesu Kristo.”


Labda ni kwa nini anaitwa mwanadamu? Mwana ni mtoto, Adamu ni mtu aliyeumbwa na Mungu, hivyo MWANADAMU ni ufupisho tu wa Mwana wa Adamu, na aliitwa hivyo kwa sababu alikuja ulimwenguni kwa njia ya kuzaliwa na mwanamke.


Na hakuna mwanadamu ambaye hahitaji kumpokea BWANA Yesu, kwani hakuna mwanadamu ambaye hana dhambi;


Warumi 3:23-24 “Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi  ulio katika Kristo Yesu.”


Na dhambi kubwa kuliko zote ni kutompokea Yesu, kutomwanini Yeye, kwani mengine yote tunahesabiwa haki katika Yeye.

Unawezaje kumpokea BWANA Yesu?


Warumi 10:9 “Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.”


Na mpango wa wokovu uliandaliwa tangu mwanzo, wakati wa uumbaji, kwani ni utaratibu wa Mungu wetu kutangaza mwisho tangu mwanzo, yaani analiandaa jambo na kuona yale yatakayotokea hadi mwisho wake, kasha anaanza kulitekeleza. Hivyo kabla hajaumba chochote, alishaona hata yale yatakayotendwa na mwanadamu atakaye muumba na mpango wa wokovu ulishaandaliwa, ndio maana Kumbukumbu la torati linafafanua zaidi kuhusu wokovu;


Kumb 26:16-19 “Leo hivi akuamuru Bwana, Mungu wako, kuzifanya amri hizi na hukumu; basi uzishike na kuzifanya kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote. Umemwungama BWANA leo, kuwa ndiye Mungu wako, na kuwa yakupasa kutembea katika njia zake, na kushika amri zake, na maagizo yake, na hukumu zake, na kusikiza sauti yake; naye BWANA amekuungama hivi leo kuwa taifa iliyotengwa iwe yake Yeye, kama alivyokuahidi, na kuwa yakupasa kushika maagizo yake yote; na kuwa atakutukuza juu ya mataifa yote aliyoyafanya, kwa sifa, na jina, na heshima, nawe upate kuwa taifa takatifu kwa BWANA, Mungu wako kama alivyosema”


Hivyo basi, kama hujampokea BWANA Yesu, tafadhali mpokee leo, huwezi kutimiza kusudi la mungu kukuumba iwapo hujampokea Yesu, kwani kumpokea Yesu ni kusudi la kwanza na muhimu kuliko mengine yote.


Kama bado hujampokea Yesu, tafadhali Kiri sala hii;

“Ee BWANA Yesu, ninakuja mbele zako, mimi mwenye dhambi, nipokee leo, nifanye kuwa wako! Lifute jina langu katika kitabu cha hukumu, niandike jina langu katika kitabu cha uzima, Nipe roho wako mtakatifu aniongoze, kutembea na wewe sawasawa, Amina.”


Kwa ukiri wa sala hii amini umeokoka, onana na kanisa lililo karibu nawe linaloamini katika wokovu kwa msaada zaidi wa kiroho au waweza wasiliana nami kwa simu namba 0713469596.

Je, hatua nyingine za kutambua kusudi la kuumbwa kwako ni zipi? Tuonane wakati mwingine.


~BARIKIWA SANA~



Friday, 17 April 2015

UNDERSTANDING THE CREATION



Hello my Dears,

Karibuni tena katika ukurasa huu unaokusudia kukupeleka katika viwango vingine katika maisha yako.

Leo tutaangalia kusudi la kuumbwa kwetu. Kila mtu Duniani ameumbwa na Mungu kwa kusudi, haijalishi ni mtu wa namna gani, ana tabia gani au anafanya nini.

Isaya 43:7 “Kila mmoja aliyeitwa kwa jina langu, niliyemwumba kwa ajili ya utukufu wangu; mimi nimemwumba, naam, mimi nimemfanya”

Je, nini kusudi la Mungu kumuumba mwanadamu? Watu wengi wanafamu tu kuwa kusudi la kuumbwa kwa mwanadamu ni ili kuzaa na kuongezeka, kuna sababu zaidi ya kuzaa na kuongezeka katika uumbaji, Majibu ya swali hili tunayapata katika uumbaji wa Mungu tukirejea katika kitabu cha Mwanzo 1:26-31; 2:8-15, ukipitia mistari hii hapo juu utafahamu kwa undani zaidi kusudi la uumbaji.

Mwanadamu alikusudiwa kuzaa na kuongezeka ili kuweza kutimiza makusudi mengine ya uumbaji ambayo ni kutawala na kutiisha, kuilima bustani na kuitunza. Uumbaji wa Mungu wote aliupa uwezo wa kuzaa na kongezeka, hivyo ili kutopoteza uwezo wa mwanadamu katika kutawala na kumiliki, Mungu aliamua kumpa  mwanadamu uwezo wa kuzaa na kuongezeka.

Embu fikiria endapo wanyama wakali wa mwituni tu ndio wangekuwa wanazaliana na kusingekuwepo na uzao kwa wanadamu ingekuwaje? Embu fikiria endapo kungekuwepo tu na mabadiliko ya hali ya nchi tu, na uwezo wa mwanadamu katika kukabiliana na mabadiliko hayo usingeongezeka, ingekuwaje? Kwa hakika ingekuwa ni tatizo kubwa.

Hivyo basi, hakuna uumbaji wa Mungu ambao haukuwa na kusudi, Je, umewahi kujiuliza ni kwa nini umeumbwa?


Kumbuka NENO linaposema kuwa umeumbwa ili kutawala na kutiisha, haina maana kuwa walio na madaraka makanisani au serikalini ndio wanaopaswa kuitimiza amri hii, sote tunategemeana, kama ambavyo Biblia inasema;

Warumi 12:4-5 “Kwa kuwa kama vile katika mwili mmoja tuna viungo vingi, wala viungo vyote havitendi kazi moja; Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja na mwenzake.”

Aliye ofisini si wathamani zaidi ya alimaye shambani na kumwezesha huyo wa ofisini kupata chakula kinachomwezesha kuishi, Raisi si wathamani zaidi kuliko askari ambao huhakikisha anakuwa salama wakati wote. Je, wewe unajishughulisha na nini?

Jambo la msingi kufahamu ni kusudi la kuumbwa kwako, Je! Umeumbwa  kwa kusudi gani?

Tukutane wakati mwingie ili kukuwezesha kutambua kusudi la kuumbwa kwako.

~Barikiwa sana~

Sunday, 12 April 2015

~WELCOME~



Dear friends;
I hearfully would like to welcome you in this page which will deal with discovering yourself and rising your faith in God and taking your path towards your destination in effective way.
This page will use English and Kiswahili languages especially for special occasions or special words.
For more information, advice and any information please contact;

E-mail; agreyndiwu@gmail.com/agrey_ndiwu@yahoo.com
Phone: +255713469596/+255765881588
WhatsApp: +255765683385
.