Tumeona hatua mbili
ambazo zitakusaidia kutambua kusudi la kuumbwa kwako, ambazo ni kwanza
kuokoka na pili historia ya maisha yako.
Wacha tuendelee kuona hatua nyingine ambayo itakuwezesha
kutambua kusudi la kuumbwa kwako;
Historia ya maisha yako/ maisha uliyopitia;
Hii ni hatua muhimu sana katika maisha ya mwanadamu,
kwani maisha uliyopitia ni sehemu ya kuandaliwa ili ulitimize lile kusudi la
Mungu katika maisha yako. Hakuna jambo a,mbalo limetokea kwa bahati mbaya
katika maisha yako, kila jambo limetokea kwa kusudi maalumu, ikiwa ni sehemu ya
kuandaliwa kwako;
Hebu tumtazame mfalme Daudi;
1Samweli 16:21 “Basi Daudi akamwendea Sauli, akasimama
mbele yake, naye akampenda sana; naye akapata kuwa mtu wa kumchukulia silaha
zake”
1Samweli 17:34-36 “Daudi akamwambia Sauli, Mtumishi wako
alikuwa akichunga kondoo za baba yake, na alipokuwa akija samba, au dubu,
akamkamata mwana kondoo wa lile kundi, mimi hutoka nikamfuata, nikampiga,
nikampokonya kinywani mwake; na akinirukia, humshika ndevu zake, nikampiga,
nikamwua. Mtumishi wako alimwua samba na dubu pia; na huyu Mfilisti
asiyetahiriwa atakuwa kama mmoja wao, kwa sababu amewatukana majeshi ya Mungu
aliye hai.”
Daudi alikuwa Mfalme maarufu sana na hodari wa vita,
ambaye alimpendeza Mungu, hata Bwana Yesu akaitwa Mwana wa Daudi. Kuwa hodari wa
vita haikuja tu kwa bahati, alipitia maisha mbalimbali ambayo yalimuandaa kwa
ajili ya jukumu hilo. Alianza kupambana na wanyama hatari waliokuwa wakivizia
mifugo yake, akaja kuwa mbeba silaha wa mfalme Sauli, hii yote ikiwa ni sehemu
ya kuandaliwa.
Hebu tumtazame pia;
Mwanzo 39:4 & 22 “Yusufu akaona neema machoni pake,
akamtumikia. Naye akamweka awe msimamizi juu ya nyumba yake, na yote yaliyomo
akayaweka mkononi mwake.” “Mkuu wa gerezaa kawatia mkononi mwa Yusufu watu wote
waliofungwa, waliomo gerezani; na yote yaliyofanyika humo ndiye aliyeyafanya.”
Utawala wa Yusufu haukuja kwa bahati tu, aliandaliwa, ni
utaratibu wa Mungu kukuandaa kabla hajakupa majukumu. Hata Musa nawe
aliandaliwa kama mtawala, kwani alichukuliwa katika familia ya kitawala (Farao)
ili awe mtawala kwa wana wa Israeli. Je, ni maisha ya namna gani umepitia? Je,
umejifunza nini katika maisha hayo? Hata kama maisha uliyopitia ni magumu kama
ambavyo Yusufu alipitia, tambua kuwa kuna kusudi la Mungu hapo, kuna jambo
unapaswa kujifunza, usipoteze wakati kwa kulaumu watu au kumlaumu Mungu, Mungu
ni Mungu wa utaratibu, hutenda kila jambo kwa kusudi maalumu, mwombe Roho
Mtakatifu akusaidie kutambua kusudi la Mungu hapo ulipo.
MAOMBI;
“Bwana Yesu, ninashukuru kwa kuniwezesha kuatmbua kuwa
maisha niliyopitia na ninayopitia yana kusudi lako ndani yake, nime Roho wako
wa Ufahamu anipe kulitambua kusudi lako na Roho wako wa Uweza anisaidie katika
kulitimiza kusudi lako. Amina.”
Usikose sehemu inayofuatia katika mwendelezo wa somo hili...
~BARIKIWA SANA~
No comments:
Post a Comment