SIRI KUBWA YA MAFANIKIO
Wapendwa wangu wakubwa wa blog hii, asante kwa kuendelea kuwa nami kwa kufuatilia masomo na jumbe mbalimbali zinazotolewa katika blog hii.
Leo nimeona ni vizuri nikawashirikisha siri hii kubwa ya mafanikio kwani imekuwa ikiwasumbua wengi na hata kuwaharibia wengine mstakabali wa maisha yao.
Nimefikia hatua hii ya kuweza kuandika ujumbe huu, kwani kwa ujumla katika maisha yangu, kuna mambo mengi sana ambayo nimekuwa nikidhamiria kwa moyo wangu yakifanikiwa, yawe makubwa au madogo.
Siri hiyo kubwa ni ipi?
1. Mwamini Mungu na mtegemee Yeye.
Neno la Mungu limetuasa sana juu ya kuwategemea wanadamu.
Yeremia 17:5 “Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana”
Kamwe usitegemee kuwa mwanadamu atakufikisha kunako mafanikio yako. Kumbuka mwanadamu anaweza kubadilika muda wowote, Mungu peke yake si kigeu geu. Ukitaka kuamini kuwa mwanadamu hawezi kukufikisha katika mafanikio yako, ngoja ufanikiwe uwe sawa nay eye au umzidi ndipo utakapotambua.
Kumbuka: Mungu huweza kumtumia mwanadamu katika kukufanikishia, usiitoe imani yako kwa Mungu.
2. Jiwekee malengo
Ili kuleta mafanikio, lazima uwe na dira inayokuongoza kuwa ni wapi unataka kuelekea. Jiwekee malengo na hakikisha unasimamia malengo yako kwa gharama yoyote ile. Utakutana na mengi katika kuyatekeleza malengo hayo, wengine wakikutia moyo na wengine wakikukatisha tamaa ila usikate tama wala kupoteza mwelekeo katika malengo yako.
Yeremia 31:21 “Jiwekee alama za njia; jifanyie miti ya kukuongoza; uuelekeze moyo wako kwenye njia kuu, njia ile ile uliyoiendea; rudi tena, Ee bikira wa Israeli, irudie hii miji yako.”
Naikumbuka kauli ya mwalimu wangu wa shule ya Msingi, Mwl Athumani Z. Ngonyani; “Kupanga ni kulazimisha mafanikio.” Itumie kauli hii, itakusaidia. Wakati wengine wanasema huwezi, wewe ng’ang’ana kuyatimiza malengo yako, waje kuona mafanikio.
3. Jiamini, amini kuwa unaweza.
Usisubiri watu wa kukutia moyo ndipo uamini kuwa unaweza, amini kuwa hadi ukawa na wazo hilo au ukawiwa kulitenda jambo hilo, ni uthibitisho tosha kuwa jambo hilo unaliweza ni saizi yako.
Hakuna mwanadamu anayetambua uwezo ulio nao, au ni jambo lipi unalihitaji, ni Mungu peke yake na wewe mwenyewe ndio mnaofahamu, acha kupoteza muda kwa kuyafuatilia maneno ya watu, yatakuchelewesha kunako mafanikio yako. Maneno yao yawe sababu ya kukuongezea juhudi katika kutekeleza mpango uliojiwekea,